Friday, January 31, 2014

Umejiunga FACEBOOK lini?? Unataka kujua umetumia muda ( siku,saa,dakika) ngapi toka ulipojiunga Facebook? Check this out!!

Takbrani miaka minne imepita mtandao wa kijamii wa Facebook umeshika kasi kubwa sana hapa nchini kiasi kwamba kama hauko kwenye mtandao huo wenye watumiaji wengi zaidi duniani basi unaonekana wewe ni wakuja.
Mtandao wa Facebook unatumika hasa kuunganisha ndugu,jamaa na marafiki wale walio karibu hata walio mbali ingawa wengine hutumia mtandao huu kwa matumizi ambayo 'siyo' kama kutukana,kutongozea,kuharibu mahusiano ya watu na kadhalika.
Kwa wanafunzi,wafanyakazi wa maofisini na hata wale wa kujiajiri,Mtandao huu hutumika kusogezea kipindi darasani hasa pale mwalimu au lecturer ama session iliyopo ni ile ya 'kuboa' au kusogeza muda wa kutoka ufike pale unapokuwa ofisini na pia kusubiria wateja au kupumzika pale unapokuwa kwenye biashara yako.
Lakini unakumbuka hasa lini umejiunga na mtandao huu,je unajua umeshapoteza muda gani kila mara unapoingia katika mtandao huu?.Je unafahamu umetumia siku ngapi,masaa mangapi,dakika ngapi na sekunde ngapi toka pale tu ulipoanza kutumia mtandao huu.
Mtandao wa kimarekani unaojulikana kwa jina la 'TimeTech' unakupa hayo mahesabu yote ndani ya dakika tano.Je unataka kujaribu na kujua muda uliotumia Facebook mpaka dakika hii?
Ingia hapa http://techland.time.com/2014/01/27/how-much-time-have-you-wasted-on-facebook/

No comments:

Post a Comment