Moja ya changamoto kubwa ya kisaikolojia kwa watu wengi duniani haijalishi watoto,vijana ama watu wazima ni kujikubali.Wengi wetu tumekuwa na wakati mgumu wa kujikubali wenyewe kuwa tunaweza kufanya jambo fulani ama kujikubali kwa hali zetu za maisha bali tumekuwa watu wa kupenda kuwakubali wengine na kujiona kuwa sisi sio kitu.
Hali hii bila kufahamu (unconsciously) imeadhiri uwezo wa watu kisaikolojia ambapo wengi wamekuwa wakifikia maamuzi yahusuyo mambo mbalimbali ya maisha yao ya kila siku ili mradi tu wapate kukubalika au kukubaliwa na mtu ama watu fulani.Hili linaweza kudhibitika kwa kuangalia maisha ya watu haswa rika la vijana walioko katika elimu ya sekondari na elimu ya juu (chuo).Wengi wamekuwa wakiishi maisha ya kuiga kutoka kwa wenzao ili wakubalike kuwa wanaenda kisasa 'digitali',pia wamekuwa wanaishi maisha yakufikirika 'fantasy' ambapo maisha hayo yamewagharimu kipato na muda mwingi.
Kwa upande mwingine,watu wenye kipato cha kawaida wamekuwa wakijiona kuwa sio watu na hawana hadhi kama watu wenye kipato cha juu.Watu hawa (kipato cha kawaida) wamekuwa na tabia ya kujidharau na kuona kuwa hawana dhamani ambayo watu wenye kipato cha juu wanacho.Hali hii imedhihirika hasa kwa wanadada wengi ambao hawana kazi ama wana kipato cha kawaida kupata wakati mgumu wa kujikubali kuwa pamoja na hali walionayo bado wanaweza kuishi maisha ya kujikubali.
Umuhimu wa kujikubali ni kuwa unakuwa huru kifkra (conscious free) na unaweza kufanya jambo lolote la maana bila kufikiri ama kujali kama watu wanaokuzunguka watalichukuliaje.Kujikubali kunakufanya ujiamini na upate ujasiri wa kusimama mbele za watu ukiamini kile ambacho ni sahihi kwako bila kujali maoni ya watu wengine kwa sababu maoni ya watu yanaweza kufanya usifikie malengo yako kwa wakati sahihi.
Kutokujibali kutakufanya usiishi maisha yako bali uishi maisha ya wengine ili kuwaridhisha marafiki,ndugu na jamaa.Kutokujikubali kunakufanya kuwa mtumwa wa maisha yako binafsi bila wewe kujua kuwa upo kifungoni.Ishi maisha ya kujikubali kutoka ndani,jikubali na jamii inayokuzunguka itakukubali tu.
No comments:
Post a Comment