Monday, September 9, 2013

“Respect yourself enough to walk away from anything that no longer serves you, grows you, or makes you happy”

Jambo kubwa ambalo limekuwa likiumiza vichwa vya watu wengi ni suala zima la mahusiano (relationships).Ingawa neno mahusiano ni pana na lina maana tofauti lakini napenda msisitizo wako kwa neno hili uwe na mlengo wa mahusiano ya kimapenzi (Love relationship).
Mahusiano ya kimapenzi ni nini?Ni pale watu wawili wa jinsia tofauti wanapofikia maamuzi ya kuwa pamoja,kufanya maamuzi ya pamoja yasiyoadhiri upande wowote kwa upendo wakiwa na lengo moja la kufunga ndoa na kuishi wote kama mke na mume baadae.
Mahusiano haya kulingana na jinsi watu walivyokutana,yanaweza kuanzia kwenye urafiki kwa muda fulani ili tu wasomane tabia baada ya hapo inafutia ile ya 'boyfriend na girlfriend thing' mahusiano haya ambayo mtu anakuwa huru kutambulisha kwa rafiki zake na hata baadhi ya ndugu kwamba huyu ndio 'boyfriend' wangu.Baada ya hapo  mahusiano rasmi ya uchumba 'courtship' ambapo wapenzi hutambulishana kwa wazazi,ndugu na jamaa huanza.
Mahusiano kwa nyakati tulizonazo sasa yamekuwa kama  'Big G' ambapo mara baada ya kutafunwa na utamu kuanza kufifia ama kuisha basi mtafunaji huitema bila kujali anaitemea wapi na kwa wakati gani.Hili huwa ni kwa pande zote mbili wanawake kwa wanaume.Pia mahusiano ya kipindi hiki yamekuwa ni ya kimaslahi zaidi kuliko hisia za kweli (True feelings) ambapo watu wamekuwa wakiingia kwenye mahusiano kwa sababu fulani ya ziada ambayo hailengi kwenye 'the ultimate goal' ya mahusiano ya mapenzi ambayo ni NDOA.
Raha ya mahusiano kwa watu wanaopendana kweli na kwa dhati ni kusikilizana kwa mambo yote yawahusuyo,kushauriana na kutoa mawazo au msaada wa maamuzi pindi mmoja anapohitaji.Zaidi ya yote mahusiano ambayo wawili huepusha kukwazana na kuishi maisha ya kutokukwaruzana kwa mambo madogo madogo,kutopelekeshana na kuridhika kwa hali iliyopo (hasa ya kipesa),mahusiano hayo hustawi na hatimaye kupelekea ndoa.
Lakini mahusiano ambayo hakuna kusikilizana,maamuzi ya mwisho ni kutoka upande mmoja kila mara,kugombana na kukwaruzana kwa sababu ndogo ndogo (Petty issues) kila siku ni mahusiano yanayoadhiri fikra na dhamira ya mtu bila kujua (Psychological torture).
Ni bora kutoka kwenye mahusiano ya hali hiyo mapema ili usiendelee kuadhirika kifkra,kiakili na pia kimwili.Mahusiano ya ambayo hakuna maelewano ama mmoja haeleweki ni bora kuyasitisha mapema ili kuepuka kuumia pindi yatakapo tokea ambayo hukutegemea.Wengi hupenda kung'ang'ania mapenzi ya kuumizwa wakitegemea mtu husika labda atabadilika siku za mbeleni na hata wengine wamedhubutu kuingia kwenye ndoa na watu wa 'dizaini' hii wakidhani eti mtu huyo huenda atabadilika akiingia ndoani lakini yale yale ama zaidi ya yale ya kuumizwa huendelea.
Mimi sio mtaalamu wa maswala ya mahusiano na mapenzi lakini nimeona na bado naona wengi wakiumizwa kwenye mapenzi na wapenzi wao na bado wamebaki kwenye mahusiano nao wakilia  mioyoni mwao kuwa mtu huyo abadilike bila mafanikio.Usifanye kosa kama hilo toka mapema na haraka kwenye mapenzi ama mahusiano ya aina hiyo kama huyo mtu hakufanyi uwe na furaha.



No comments:

Post a Comment